Friday, February 14, 2014

AZAM WAENDELEA KUJIFUA MSUMBIIJI KUCHEZA JUMAPIL

Posted By: Unknown - 7:52 PM

Share

& Comment

Wawakilishi wa Tanzania katika kombe la Shirikisho barani Afrika, timu ya Azam inaonenakana kujiandaa kikamilifu kukabiliana na hali ya hewa ya hapa Beira ikiwemo kuwa tayari kucheza huku mvua kubwa ikinyesha.

Azam iko hapa tangu Jumatano ikijitayarisha vilivyo na pambanao la marudiano dhidi ya wenyeji Ferroviario da Beira litalokafanyika kwenye uwanja wa wenyeji hao siku ya Jumapili kuanzia saa 9 alasiri za Msumbiji (saa 10 za Tanzania)

Wawakilishi hao wa nchi wanahitaji ushind au sare kutokana na ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam.

Hapo jana Alhamis, timu ilifanya mazoezi mara mbili; asubuhi kwenye uwanja litalapopigwa pambano Jumapili huku sehemu ya mazoezi ikiwa wakati wa mvua na jioni mazoezi yalihamishiwa kwenye uwanja mwingine ambapo pamoja na kwamba mvua ilikuwa imekatika kwa muda, sehemu kubwa ya uwanja ilijaa maji. Hata hivyo hali hiyo haikuzuia mazoezi kufanyika na ratiba ilikwenda kama ilivyopangwa ili kuzoea mazingira na uhalisia wa hali ya hewa.

Kwa mujibu kiongozi wa jumuia ya watanzania wanaoishi hapa Msumbiji, Richard Alloyce hiki ni kipindi cha majira ya vuli ambapo mvua hunyesha kuanzia Desemba hadi mwishoni mwa Februari.

"Ni kawaida kuwa na mvua kipindi hiki, inanyesha siku mbili au tatu kisha jua linatoka kwa siku mbili na baadaye mvua inaendelea, tena hii si mvua kubwa, ipo ile ya masika ambayo inatarajiwa kuanza mwezi Machi hadi mwanzoni mwa Juni ikifuatiwa na kipindi cha baridi kali kama ilivyo sehemu kadhaa za kule kwetu Tanzania, alibainisha Alloyce ambaye ameishi Msumbiji kwa miaka 11 sasa.

Pamoja na maelezo hayo ya mwenyeji kwa upande mwingine alikiri kuwa yawezekana kukawa na mabadiliko kidigo kutokana na kiwango cha mvua inayonyesha hivi sasa kwani ni kubwa tofauti na miaka iliyopita mbapo hudodndoka manyunyu tu na kufuatiwa na jua la wastani.

Kulingana na taarifa za mamlaka ya hali ya hewa hapa Msumbiji, mvua inatarajiwa kuendelea kunyesha kwa muda wa siku tatu hadi Jumapili ambayo ni siku ya mchezo.

Usiku wa kuamkia leo mvua kubwa imekuwa ikipiga usiku mzima na inaendelea kupiga hata hivi sasa.Jua halijaonekana kwa siku ya pili.

Leo Mkufunzi Joseph Omog amepanga timu yake ifanye mazoezi mara moja majira ya saa 9 za hapa, na hivyo kuna kila dalili kuwa mazoezi hayo yatafanyika wakati wa mvua.

Katibu Mkuu wa Azam FC Nassor Idrissa anasema kulinagana na taarifa zilizokuwa zimepatikana mapema uongozi ulikuwa na dondoo za hali ya hewa ya Beira na hivyo matayarisho muhimu yalifanyika kwa upande wa vifaa hususan uwepo wa viatu maalum vya kuchezea katika sehemu yenye unyevunyevu ili kuhimili utelezi na hatimaye kupata matokeo yanayohitajika.

"Tulishakumbana na hali kama hii wakati fulani nchini Uganda wakati tuanajitayarisha na ligi, mazingira yalikuwa magumu sana na tulijikuta tunapigwa na Bunamwaya (timu ya Uganda inayoshiriki ligi kuu) goli 4 kabla ya mapumziko, kutokana na wachezaji kuteleza ovyo lakini baada ya kubadili viatu tulifanikiwa kurejesha magoli yote na tukapata sare ya 4-4, tokea hapo tumekuwa na tahadhari kubwa ya mambo haya"alinena Idrissa ambaye ni maarufu kwa jina la "Father"

Ujumbe mzima wa Azam FC umefikia katika hotel ya Rainbow Mozambique yenye hadhi ya nyota tatu (3).

Mchezo wa Jumapili umepangwa kuchezeshwa na waamuzi kutoka Zambia na ikiwa Azam itafaulu kusonga mbele itakabiliana na timu ya Shirika la Umeme la Zambia, Zesco kati ya Machi 1 na 2 jijini Dar es Salaam na kurudiana juma moja baadaye mjini Ndola.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.