Sunday, February 16, 2014

OMOG: LENGO LA MCHEZO WA LEO NI KUFUZU TU

Posted By: Unknown - 6:35 AM

Share

& Comment

https://fbcdn-photos-f-a.akamaihd.net/hphotos-ak-prn2/t1/p600x600/1497320_705274822846210_2073843781_n.jpg
WACHEZAJI WA AZAM FC BAADA YA MOJA YA MAZOEZI NCHINI MSUMBIJI
N a Florian Kaijage, Beira

Kocha Mkuu wa Azam Joseph Omog amesema timu yake itaingia dimbani kuwakabili wenyeji Jumapili Ferroviario da Beira kwa lengo moja tu la kufuzu kwa raundi inayofuatia katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Omog amesema matayarisho yote yamekwenda sawa katika muda wa siku tatu ambazo wamekuwa hapa Beira na kubainisha kuwa wachezajin wake wote wako katika hali nzuri kwa ajili ya mchezo huo muhimu wa marejeano.

“Tumefanya mazoezi kwa siku tatu, hatuna matatizo makubwa ya kutukwaza, jambo pekee ambalo si sawa ni hali ya mvua ambayo imesababisha viwanja kujaa maji, kwakuwa Jumamosi mvua haikunyesha ni matarajio kuwa hata Jumapili hapatakuwepo mvua ili uwanja uwe katika hali nzuri kuhimili mchezo” alibainisha Omog.

Huku akitambua changamoto inayoikabili timu yake katika mchezo huu wa marejeano baada ya kupata ushindi wa 1-0 la Kipre Tchetche Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam, kocha Omog amesema wanachukua tahadhali zote kimchezo kwa kuwaelekeza wachezaji wake wanacheza kwa lengo la kupata magoli na iwapo magoli yatashindikana basi wazuie kwa umoja na kuepuka kuruhusu goli langoni mwao.

“Mpango ni kuhakikisha tunamiliki mpira kuliko wapinzani wetu, tunaponyang’anywa mpira lazima tujitahidi kuurejkesha mpira kwenye miliki yetu mapema iwezekanavyo nah ii ni kazi ya timu nzima ambayo itatuwezesha kutimiza malengo yetu” alinena mkufunzi huyo bingwa wa kombe la Shirikisho mwaka jana akiwa na klabu ya AC Leopards ya Kongo Brazaville.

Kuhusu utelezi uwanjani amabao unaweza kuvuruga mipango ya timu yake Omogo alisema maelekezo kwa wachezaji wake hususan wa safu ya ulinzi ni kuhakiksha hawaruhusu mipira kuzagaa katika eneo lao, hivyo lazima waihamisha haraka kuepusha hatari.

Aliongeza kuwa baada ya kuwaona wapinzani wao katika mchezo wa kwanza, amebaini kuwa wanapendelea kutumia mipira mirefu, hivyo amesema hilo ni eneo lingine muhimu ambalo amelitilia mkazo wakati wa mazoezi.

Kikosi kilichoanza mchezo wa kwanza kilikuwa Mwadini Ally, ni Erasto Nyoni, Malika Ndeule, Aggrey Morris Said Morad, Michael Bolou, Himid Mao, Salum Abubakar Brian Umony, Kipre Tchethche na Mcha Hamis.

Bado mwalimu Omog anazo bunduki zake nyingine kama nahodha John Bocco ambaye amerejea kutoka majeruhi na Dar es Salaam aliingia kipindi cha pili. Pia wapo Jabir Aziz aliyecheza pia kipindi cha pili, David Mwantika ambaye hakucheza mchezo wa kwanza kwa kuwa alikuwa akitumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoonesha kwenye wa mwaka jna dhidi ya FAR Rabat ya Morocco na nyota wengineo.

Mchezo huu wa marejeano kati ya Ferroviario Beira na Azam utafanyika katika uwanja unaomilikiwa na Ferroviariona ambao unauwezo wa kubeba watazamaji elfu tisa.

Kipute hicho kitaanza saa 9 alasiri za Msumbiji sawa na saa 10 za Afrika Mashariki na waamuzi wanatoka Zambia wakiongozwa na mwamuzi wa kati, Wisdom Chewe. Kamishna wa mchezo ni Charles Kafatia wa Malawi.

Jumuiya ya Watanzania waishio hapa Msumbiji wakiongozwa na Richard Alloyce wamejipanga vilivyo kuishangilia Azam na wamekuwa wamsaada mkubwa kuelekea mchezo huo.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano, dakika 90 zikimalizika bila mshindi kuamuliwa, itatumika changamoto ya mikwaju ya penati. Omog amesema timu yake imejiandaa kwa mazingira yote.

Iwapo Azam itafaulu kuitoa Ferroviario itakabiliana na Zesco ya Zambia,ikianzia nyumbani kati ya Machi 1 na 2 mwaka huu.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.