Wednesday, March 26, 2014

AZAM MWENDO MDUNDO, BOCCO KAMA KAWA

Posted By: kj - 8:07 PM

Share

& Comment


 

Vinara wa ligi kuu ya ya vodacom Azam FC wameendeleza wimbi lao la ushindi huku mfungaji bora wa wakati wote wa Azam FC John Raphael Bocco akiendelea kufumania nyavu za timu pinzani.

Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Mgambo JKT, Azam FC wameibuka na ushindi wa goli 2-0.

Kwa mara ya kwanza kocha Omog aliwanzisha kwa pamoja washambuliaji John Bocco na Gaudenci Mwaikimba katika safu ya ushambuliji ambapo ilidumu kwa dakika 53, kabla ya Mwaikimba kwenda benchi na kumpisha Brian Umony katika dakika ya 53.

Dakika 10 baada ya Brian Umonyi kuingia Azam FC waliandika goli la kuongoza kupitia kwa nahodha John Bocco akiunga pasi ya Brian Umonyi.

Brian Umonyi alihitimisha ushindi wa Azam FC wa goli 2-0 katika uwanja huo wa Mkwakwani kwa kuifungia Azam FC goli la pili katika dakika 82 kwa shuti kali ambalo lilimbabatiza kipa Salehe Tendega na kuingia nyavuni.

Kwa matokeo hayo ya leo Azam FC wanaendelea kuongoza ligi kwa tofauti wa pointi 4 kwa kufikisha pointi 50 huku yanga wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 46.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Gaudence Mwaikimba/Brian Umony dk53 , John Bocco ‘Adebayor’ na Kipre Tchetche/Waziri Salum dk81.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.