Azam FC iliandika goli lake la kwanza kupitia kwa Hamisi Mcha Viali katika dakika ya 17 kabla ya Joseph Owino aliyepata kuitumikia Azam FC kipindi cha nyuma kuisawazishia Simba SC katika dakika ya 45 na kupelekea mchezo kwenda mapumziko wakiwa sre ya goli 1-1.
Katika kipindi cha pili Azam FC walirejea kwa kasi huku wakisaka goli la ushindi lililofungwa nanahodha John Bocco kwa kichwa akiunga mpira uliogonga mwamba kufuatia shuti la Kipre Hermani Tcheche.
Goli la John Bocco liliihakikishia Azam FC ushindi wa goli 2-1 na hivyo kujikusanyia pointi 53 baada ya kucheza michezo 23 na kuiwacha Yanga wakibakiwa na pointi zao 46 baada ya leo kukubali kichapo cha goli 2-1 baada ya kucheza michezo 22.
Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Aggrey Morris, David Mwantika, Kipre Balou, Himid Mao/Bryson Raphael dk75 , Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’, Kipre Tchetche/Brian Umony dk80 na Khamis Mcha ‘Vialli’/Kevin Friday dk55.
0 Maoni:
Post a Comment