Sunday, March 23, 2014

BOCCO AIPAISHA AZAM

Posted By: Unknown - 6:36 PM

Share

& Comment

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/05/John-Boko-Azam-fc1.jpg
Azam FC imefanikiwa kuvuna pointi zote tatu hii leo mbele ya JKT Oljoro katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Azam Complexs uliopo Mbande nnje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Azam FC katika mchezo wa leo waliwaanzisha wachezaji wa tatu toka kikosi cha pili "Azam Academy" ambao ni Aishi Salum Manula, Raphael Bryson na Gadiel Michael huku wakifanikiwa kupata goli 1 pekee katika mchezo wa leo.

Azam FC ilibidi wangoje mpaka dakika ya 72 ambapo nahodha John Raphael Bocco aliiandikia Azam FC goli pekee la ushindi katika mchezo huo wa leo.

Leo Azam FC walikosa huduma ya kiungo Kipre Bolue pamoja na beki Erasto Nyoni aliyezawadiwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita dhidi ya Yanga huku majeruhi Waziri Salum akiwa benchi ikiashiria kupona kwa majeraha yake na huenda kuanzi mchezo ujao akaanza kuonekana tena.

Kwa matokeo ya mchezo wa leo wa goli 1-0 umepelekea Azam FC Kufikisha point 47 wakiwa mbele kwa pointi 4 dhidi ya Yanga wenye pointi 43.

Kikosi cha Azam kilichoanza leo ni: Aishi Manula, Himid Mao, Gardiel Michael, Saidi Moradi, David Mwantika, Raphael Bryson, Salum Aboubakari, Hamisi Mcha, Brayn Omonyi, John Bocco, Kipre Tcheche.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.