Sunday, March 23, 2014

TCHECHE: UBINGA UTATUWA CHAMANZI

Posted By: Unknown - 3:34 PM

Share

& Comment

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, raia wa Ivory Coast, Kipre Tchetche amesema pamoja na ubora wa kikosi cha Yanga, timu hiyo ina safu ya ulinzi nyepesi inayopitika kirahisi.

Tchetche mfungaji bora wa msimu uliopita, alisema kutokana na udhaifu iliokuwa nayo timu hiyo, hafikirii kama wanaweza kutetea ubingwa wao kwa sababu bado wana mechi ngumu dhidi ya Kagera Sugar na wapinzani wao, Simba.

“Ni timu nzuri lakini ambayo ina wachezaji wenye uwezo mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji na kiungo, lakini ni dhaifu kwenye ulinzi wake ndiyo maana niliwasumbua sana hadi tukaweza kusawazisha bao walilotufunga kipindi cha kwanza,” alisema Tchetche. Yanga na Azam zilikutana Jumatano iliyopita na kutoka sare ya bao 1-1.

Akizungumzia mwenendo wa timu yake ya Azam, Tchetche alisema wana nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa kwa mara ya kwanza kutokana na nafasi waliyopo hivi sasa ukilinganisha na mabingwa watetezi, Yanga.

“Tunayo nafasi ya kurekebisha makosa yetu ambayo tumeyafanya kwenye misimu miwili ya kumaliza nafasi ya pili na sasa kutwaa ubingwa wa Tanzania kwa mara ya kwanza, lakini hili litawezekana endapo tutaendelea kujituma hadi siku ya mwisho kwa sababu ushindi uliopo kwa sasa ni mkubwa,” alisema Tchetche.

Tchetche aliyejiunga na Azam FC misimu mitatu iliyopita akitokea timu ya JCE inayoshiriki ligi kuu ya Ivory Coast, amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho.


CHANZO: HABARI LEO

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.