Wednesday, April 16, 2014

AZAM WAANZA KUIVUTIA KASI JKT RUVU

Posted By: Unknown - 12:16 PM

Share

& Comment

AZAM FC inaanza mazoezi leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam baada ya mapumziko ya siku moja, tangu wachezaji wa timu hiyo warejee kutoka Mbeya ambako walitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa wiki.

Azam inatarajiwa kucheza mechi ya mwisho ya kukamilisha msimu wa ligi Jumamosi Uwanja wa Azam Complex dhidi ya JKT Ruvu, siku ambayo pia watakabidhiwa taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu.


Mamia ya mashabiki walijitokeza kwa wingi Jumatatu jioni ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam kuilaki timu yao, ikitokea Mbeya ambako jana iliifunga Mbeya City na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.


Msafara wa wa Azam uliwasili kwa ndege ya Fats Jet Saa 12:00 jioni na kupokewa na mamia ya wapenzi wake kabla ya kupanda basi lao la kisasa kuelekea makao yao makuu, Azam Complex, Chamazi.


Ilikuwa hoi hoi, nderemo na vifijo katika mapokezi ya timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake katika mapokezi yake baada ya mabingwa hao wapya wa Bara kutua JNIA.


Azam ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Jumapili, baada ya kuifunga Mbeya City mabao 2-1 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, huku waliokuwa wapinzani wao katika mbio za taji hilo, Yanga SC wakishinda 2-1 dhidi ya JKT Oljoro mjini Arusha.


Azam imefikisha pointi 59 ikiwa na mchezo mmoja mkononi ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote baada ya mechi za mwisho Aprili 19, mwaka huu. Yanga SC yenye pointi 55 sasa ikiifunga Simba SC wiki ijayo itafikisha 58.


Licha ya kuwa timu ya kwanza kuifunga Mbeya City kwenye Uwanja wake Aprili 13, mwaka huu, Azam FC pia inakuwa timu ya kwanza nje ya Simba na Yanga kutwaa ubingwa wa Bara tangu mwaka 2000 Mtibwa Sugar ilipofanya hivyo


Azam inakuwa timu ya saba nje ya Simba SC kutwaa taji la Ligi Kuu, baada ya Cosmo mwaka 1967, Mseto mwaka 1975, Pan Africans mwaka 1982, Tukuyu Stars mwaka 1986, Coastal Union 1988 na Mtibwa Sugar mara mbili mfululizo 1999 na 2000.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.