Tuesday, April 1, 2014

RUVU SHOOTING NA AZAM KUCHEZWA APRIL 9

Posted By: kj - 8:55 PM

Share

& Comment

MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Azam FC na wenyeji Ruvu Shooting uliokuwa ufanyike Aprili 6, mwaka huu Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani umesogezwa mbele hadi Aprili 9, imefahamika.  

Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ ameiambia tovuti ya klabu kwamba, sababu za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuusogeza mbele mchezo huo ni Azam FC kuwa na wachezaji wengi katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes. 

Ngorongoro Heroes inatarajiwa kuondoka keshokutwa nchini kwenda Nairobi, Kenya kwa ajili ya mechi ya kuwania kucheza Fainali za Vijana Afrika, itakayochezwa Jumapili ya Aprili 6 mwaka huu Uwanja wa Machakos ulioko kilometa 80 kutoka jijini Nairobi na Azam ina wachezaji zaidi ya watano kwenye kikosi hicho. Hao ni Aishi Manula, Bryson Raphael, Gardiel Michael, Kevin Friday, Mudathir Yahya, Farid Mussa na Hamad Juma.  

Wachezaji waliobaki wa Azam FC wanaendelea na mazoezi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Azam FC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 53 baada ya kucheza mechi 23, ikifuatiwa na Yanga SC yenye pointi 46 za mechi 22 na Mbeya City yenye pointi 45 za mechi 23.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.