Thursday, June 5, 2014

SURE BOY AKANA KUJIUNGA NA YANGA

Posted By: kj - 11:37 PM

Share

& Comment

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjueqt7hcYpEj8QHTnbzreOESTZriRx01Rf7Q37zNzCTMB9h6NfOdyF3NoXFD8eF2HGhz5wfdin8VytaPSCpf_bOWEoTKu6EyiJZJTHtMwdW4KGgr56Hs5yJvtAfHbRTagfxp9RivyDTt8/s400/sure+boy.jpg
KIUNGO mchezeshaji wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amesikia taarifa za kujiunga na Yanga lakini akacheka na kusema kwa sasa hilo ni gumu hata ikimleta kocha wa maana kama Marcio Maximo.
Sure Boy ambaye ni mtoto wa winga wa zamani wa Yanga, Abubakar Salum alisema; “Nasikia taarifa nyingi kuwa nimeonekana Yanga mara nimesaini nao, zimenishangaza sana lakini hii ndiyo nchi yetu mimi bado mchezaji halali wa Azam nipo sana hapa na nina furaha ya kuwa hapa.”
“Naheshimu mkataba wangu ambao nimebakiza Azam, hatuwezi kujua nini kitatokea huko mbele ya safari,”alisisitiza mchezaji huyo mwenye mkataba wa mwaka mmoja na nusu Azam.


CHANZO: MWANASPOTI

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.