Saturday, June 14, 2014

KAVUMBAGU, BOLUE, TCHECHE KUANZA MAZOEZI JUMATATU

Posted By: kj - 10:18 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam fc wanatarajia kuanza mazoezi ya
maandalizi wa msimu uliopita jumatatu, ambapo mastaa wote watakuwa
Chamanzi.

Meneja wa azam fc Jemedari Said amesema kuwa wachezaji wote wanatakiwa
kuripoti katika mazoezi hayo isipokuwa wale waliopo katika kambi ya
taifa stars.

"Wachezaji wote wanatakiwa kuwasili kwa ajili ya kuanza mazoezi
jumatatu, hayo ndiyo makubaliano tuliyofikia wakati tunavunja kambi
aprili, haijalishi anatoka wapi na alikuwa anafanya nini, kila
mchezaji anatakiwa kuwasili,"alisema Jemedari.

Jemedari ameongeza kuwa: "mpaka sasa sina taarifa yoyote ya udhuru wa
mchezaji, hivyo nategemea wachezaji wote watawasili isipokuwa wale
walioko kwenye timu za taifa, kocha Omog atawasili tarehe 20 ila kwa
siku za mwanzo wachezaji wetu watafanya mazoezi chini ya makocha
wasaidizi".

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.