Mchezo huo wa robo fainali ulishuhudia kikosi cha pili cha Simba SC na Azam academic zikimaliza dakika 90 wakiwa sare ya bila kufungana na mikwaju ya penati ikaivusha Azam academic.
Azam Academic walifanikwa kupata penati 3 wakati Simba SC wakipata penati mbili, huku penati za Azam academic zilizotinga nyavuni zikiwa zimefungwa na Kassim Kisengo, Adam Omar na Reyna Mngungila.
Azam academic leo watacheza na Enyima katika mchezo wa nusu fainali ya pili utakao anza saa kumi jioni katika uwanja wa Azam complex.
PICHA ZA MCHEZO WAJANA KUTOKA KWA BIN ZUBEIRY
Mchezaji wa Azam FC, Sadallah Mohamed kulia akichuana na Aziz wa Simba |
Mshambuliaji Jamal Mchaulu 'Balotelli' wa Azam FC akimiliki mpira mbele ya beki wa Simba SC, Omar Hussein |
Mchezaji wa Azam FC, Christopher Mshanga kulia akimtoka mchezaji wa Simba, Omar Hussein |
Wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Simba SC, Amisi Tambwe na Shaaban Kisiga walikuwepo Karume kushuhudia wadogo zao |
Kiungo wa Azam FC, Malik Mussa kushoto akimtoka beki wa Simba SC, Mbaraka Yussuf |
Mchezaji wa Azam FC, Adam Omar akimuacha chini mchezaji wa Simba |
Kocha Mkuu wa Azam FC, Mcameroon Joseph Marius Omog alikuwepo |
Kocha Mkuu wa Simba SC, Mcroatia Zradvko Logarusic (katikati) alikuwepo |
0 Maoni:
Post a Comment