Thursday, July 3, 2014

AZAM: HATUJAMSAJILI CHUJI, KAOMBA KUFANYA MAZOEZI

Posted By: Unknown - 10:17 PM

Share

& Comment

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqUGzfUmJ1T6m2fc9SxDgcKOft2bZTygMrKy-Uz_SQwWzT6_C434wnk7mAjjDBqDMnjHiyekgeJK15pXNxpkFg0qzPI-MlQOif2vCUTZCYDM1Agcb29T3lIKBYZAj4e1FLOgBByY_n8NL2/s1600/CHUJII.jpg
Mabingwa wa Tanzania Bara Azam FC wamekanusha taarifa za kumsajili kiungo aliyetemwa kutoka Yanga Athumani Iddi Chuji, baada ya taarifa zilizo enea hii leo ya kuwa amepewa mkataba wa mieazi 6.


Uvumi wa Chuji kusajiliwa Azam FC umeibuka baada ya kuonekana hii leo akifanya mazoezi na Azam FC katika uwanja wa Azam Complex, kama katika picha hapo juu inavyomuonyesha.

Msemaji wa Azam FC, Japhari Iddi Maganga amesema kuwa Chuji ajaingia mkataba wowote na Azam FC mpaka kufikia jioni ya leo, na wataingia nae mkataba endapo kocha Omog akiridhika na kiwango chake.

Maganga alisema kuwa Chuji anaesifika kwa kupiga pasi ndefu, aliomba kwa uongozi wa Azam FC kufanya mazoezi na timu ya Azam FC, na baada ya uongoz kuongea na kocha Omog ambay aliridhia kwa Chuji kufanya mazoezi na timu yake, walimruhusu na leo akaanza mazoezi.

Maganga aliongeza kuwa endapo kocha ataridhia kiwango chake katika mazoezi hayo na akataka asajiliwe basi uongozi utampatia mkataba Chuji.

Athumani Iddi ni miongoni mwa wachezaji waliotemwa na Yanga na hivi sasa bado haja pata timu japo kuwa aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Yanga Minziro ameonyesha nia ya kumuhitaji katika timu yake ya JKT Ruvu.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.