Thursday, July 3, 2014

AZAM KUAMUA MAHALI PA KAMBI JUMATATU

Posted By: Unknown - 5:59 AM

Share

& Comment

UONGOZI wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Azam FC, unatarajia kukutana Jumatatu ya wiki ijayo, kujadili mapendekezo ya Kocha wao Mkuu, Joseph Omog juu ya sehemu ya kuweka kambi na mengineyo.

Omog aliipa Azam FC ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita licha ya kludumu nayo kwa kipindi kifupi tangu apokee kijiti kutoka kwa aliyekuwa mtangulizi wake, Mwingereza Stewart Hall.

Habari kutoka ndani ya uongozi wa Azam, mbali ya suala la kambi, Omog amependekeza mambo mengi, hivyo wanakutana kujadili ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu.

Kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita, mbali ya kibarua cha kuutetea, pia anakabiliwa na kazi ya kuiandaa timu kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kati ya mapendekezo yake, Omog ameutaka uongozi kuipeleka timu walau wiki mbili nchini Afrika Kusini au Hispania kabla ya kurejea kuanza kibarua cha Ligi Kuu itakayoanza mwishoni mwa mwezi ujao.

“Tumepokea mapendekezo ya kocha, ni mazuri ila sisi tunatakiwa kukaa kuyapitia ili kutoa uamuzi wa nini kifanyike, hivyo Jumatatu ijayo tutaketi kujadili mapendekezo yake,” kilidokeza chanzo hicho.

Azam iliyoanzishwa Juni 24, 2007, itashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa mapema mwakani kwa mara ya kwanza baada ya kucheza mara mbili mfululizo Kombe la Shirikisho.



CHANZO: TANZANIA DAIMA

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.