Friday, June 20, 2014

KIMWAGA NNJE YA UWANJA MIEZI 9, APASULIWA GOTI LA KUSHOTO

Posted By: kj - 5:32 PM

Share

& Comment

Mshambuliaji chipukizi wa Azam fc Joseph Kimwaga anatarajiwa kukaa
nnje ya uwanja kwa takribani miezi 9 kutokana na upasuaji wa goti
utakao fanywa leo nchini Afrika Kusini.

Kimwaga ambaye aliifungia Azam fc katika ushindi wa goli 3-2 dhidi ya
yanga amekuwa akisumbuliwa na goti toka mwezi february mwaka huu na
kupelekea kushindwa kumalizia msimu uliopita ambao Azam fc walitwa
ubingwa.

"Kimwaga atafanyiwa upasuaji wa goti la mguu wa kushoto leo na baada
ya upasuagji huo atapumzishwa kwa muda wa wiki moja Afrika kusini
halafu atarudi Dar es salaam," alisema daktari wa azam fc, Dr Mwanandi
Mwankemwa.

Mwankemwa aliongeza kuwa; "Baada ya kurudi atakaa nje ya uwanja kwa
muda wa miezi 9 hadi atakapopona kabisa na kuanza mazoezi mepesi
kurudia hali yakd ya kawaida."

Kimwaga ni miongoni mwa wachezaji waliotokea Azam academy
waliyoisaidia azam fc kutwa taji lao la kwanza la ligi kuu ya vodacom.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.