Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa Azam FC, Joseph Omog alisema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo wa Jumapili na faraja kubwa kwake ni kurudi dimbani kwa beki wake kisiki, Aggrey Moris aliyekuwa akisumbuliwa na malaria yalisababisha ashindwe kusafiri na timu ya taifa ‘Taifa Stars’.
“Kwa ujumla
tumeshamaliza maandalizi na kikosi changu kipo tayari kwa ajili ya
mchezo na Yanga pamoja na Ligi Kuu kwa sasa sina majeruhi baada ya Moris
kuanza mazoezi leo (jana) na Jumatano, Didier Kavumbagu atakuwa amerudi
kutoka kumaliza majukumu yake ya timu yake ya taifa,” alisema Omog.
Ukiacha kurejea uwanjani kwa nyota hao, Omog alisema anafurahi kuona mshambuliaji raia wa Haiti, Lionel Saint Preux anaendelea vizuri na mazoezi baada ya kuumia goti wakati akiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo Azam Complex.
Beki kisiki Agrey Morice |
Hiyo ni mara ya pili kwa timu hizo kucheza mechi ya Ngao ya Jamii ambapo msimu uliopita timu hizo zilikutana na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa katika dakika ya pili na kiungo Salum Telela.
chanzo: habari keo
0 Maoni:
Post a Comment