Sunday, September 7, 2014

AZAM WASHUSHA KIFAA CHA KUPIMA UFANISI WA WACHEZAJI

Posted By: Unknown - 5:55 AM

Share

& Comment

http://www.mwanaspoti.co.tz/image/view/-/2443352/highRes/824331/-/maxw/600/-/di1q8vz/-/azam12.gif
UNAKUMBUKA wakati fulani yule kocha Mholanzi wa Yanga, Hans Pluijm, alishauri kinunuliwe kifaa fulani hivi cha mfumo wa elektroniki kwa ajili ya kupima ufanisi wa wachezaji wake uwanjani?

Ishu hiyo ikayeyuka Yanga baada ya jamaa kutemwa. Sasa matajiri wa Azam FC wamekishusha kifaa hicho nchini na kimeanza kufanya kazi.

Klabu hiyo pekee Afrika Mashariki ambayo uwanja wake binafsi unakubalika kwa mechi za kimataifa, sasa inasubiri programu maalumu ya Kijerumani ambayo itaunganishwa na kifaa hicho cha ‘Vis.Track Gps’ ambacho itakitumia kujua ufanisi wa kila mchezaji wake uwanjani.

Vis.Track Gps kazi yake kubwa ni kupima takwimu za ufanisi wa mchezaji kuanzia mazoezini mpaka kwenye mechi.

Kwa mujibu wa Meneja wa Azam, Jemedari Said, programu hiyo imeletwa na kocha wa vijana aliyekuwa anafanya mazoezi ya vitendo katika klabu hiyo aitwaye Soren Lurz, raia wa Ujerumani.

“Soren ametupatia programu ambayo itatuwezesha kufahamu ufanisi wa kila mchezaji uwanjani, hii tutaitumia haraka iwezekanavyo pengine hata kabla ya ligi kuanza,” alisema Jemedari.

“Kila baada ya mechi tutakuwa tunafanya tathmini kwa kutumia taarifa kutoka kwenye kompyuta hapo tutajua kila kitu na kukifanyia kazi kiufundi.”

Alisema kifaa hicho kitatoa taarifa ya umbali aliokimbia mchezaji uwanjani, muda aliokaa na mpira na idadi ya mashuti aliyopiga hivyo kila mchezaji atajua utendaji wake.

Kifaa cha Vis.Track Gps kinaweza kupachikwa katika jezi ya mchezaji au taarifa kuingizwa katika kompyuta na kumfuatilia kila mchezaji uwanjani. Klabu nyingi za Ulaya hutumia teknolojia hii kupima ufanisi wa mchezaji uwanjani.

Awali Yanga ilikuwa na mpango wa kutumia kifaa hicho chini ya Pluijm lakini mpango huo uliyeyuka baada ya kocha huyo kutemwa.



chanzo: mwanaspotia

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.