Nahodha wa mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom John Raphael Bocco anataraji kukosa mchezo wa ngao ya jamii na michezo mitatu ya ligi kuu ya vodacom.
Kwa mujibu wa taarifa iliyo wekwa katika ukurasa wa Azam FC inaeleza kuwa John Bocco ametakiwa kukaa nnje ya uwanja kwa wiki tatu kuanzia sasa na kumplekea kukosa michezo hiyo minne (mitatu ligi kuu na mmoja ngao ya jamii).
"Captain John Bocco pamoja na jana kufanya mazoezi katika Gym ya kisasa pale Chamazi - Azam Complex, lakini vipimo alivofanyiwa mchana na mtaalamu (physiotherapist) Gilbert Kigade pale Msasani Peninsula Hospital ili kuangalia maendeleo yake, alibainisha kwamba Bocco anatakiwa apumzike kwa wiki 3 huku akipata matibabu. Bocco anasumbuliwa na maumivu ya misuli na hivyo ataikosa mechi ya Jumapaili dhidi ya Yanga na pia michezo 3 ya mwanzo ya Ligi kuu ya Vodacom." ilielza taarifa hiyo.
Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Azam FC kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii kwani ilipoteza kwa Simba mwaka 2012 na mwaka 2013 ikapoteza tena kwa Yanga.
0 Maoni:
Post a Comment