Saturday, September 13, 2014

AZAM KUENDELEZA UBABE KESHO?

Posted By: Unknown - 2:32 PM

Share

& Comment


Ni wakati mwingine bazia la msimu mpya wa ligi Tanzania Bara unafunguliwa kwa kuwakutanisha kwa mara nyingine tene Azam FC ambao ni mabingwa wa Tanzania Bara dhidi ya makanu bingwa Yanga katika uwanja wa taifa hapo kesho.

 Mchezo huo unaongojwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini unataraji kuanza saa kumi jioni ambapo tiketi zake zimeanza kuuzwa kwa njia ya mpesa.

Yanga na Azam FC walikutana katika ngao ya jamii msimu uliopita ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa goli 1-0, baada ya mchezo huo Azam FC haijapoteza tena mchezo wowote wa ushindani dhidi ya timu za Tanzania.
http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/12/AzamFC.jpg
Chini ya Kocha Omog ambaye alirithi mikoba ya Stewart Hall mwishoni mwa mwaka jana, Azam FC imepoteza michezo mitatu dhidi ya KCC ya Uganda katika michuano ya kombe la Mapinduzi, dhid ya FERROVIARIO Da BEIRA ya Msumbiji na dhidi ya El-merekh ya Sudan.

Wakati yanga baada ya mchezo huo ilipoteza michezo miwili katika ligi na mmoja dhidi ya Simba katika tamasha la mtani jembe.
 http://api.ning.com/files/gWhc*8EYmk-iJK-8XgA0i286-jL3IzcBGhKwwCXvLNkdlAOCT-362WBkTeNKGw1p2vdXRa62RItSLkwsZgOiiAEt3acqeWcf/yanga.JPG
Yanga chini ya kocha Marcio Maximo bado haija cheza mchezo wowote wa ushindani na mchezo dhidi ya Azam utakuwa mchezo wake wa kwanza huku katika michezo ya kirafiki aliyoiongoza Marcio Maximo yanga imeshinda michezo yote.

Mashabiki wa Yanga wanangoja kwa hamu kushuhudia timu yao inakuwa ya kwanza kuifunga Azam iliyo chini ya Omog kwa timu za Tanzania, baada ya kwenye mchezo wa ligi mzunguko wa pili msimu uliopita kushindwa kufanya hivyo wakatu Azam FC wakiwa pungufu.

Wakati mashabiki wa Azam FC wanaosuburi kwa hamu kushuhudia kikosi chao kikiendeleza ubabe wake kwa timu za Tanzania walio aanza kuuonyesha toka msimu uliopita na kutwaa ngao ya hisani kwa mara ya kwanza baada ya kufanikiwa kucheza mara mbili mfululizo na kushindwa kuitwaa.

Yanga huenda wakamkosa kiungo wao toka Btazili Continhoo katika mchezo wa kesho ambapo Azam FC watakosa nahodha wao John Raphael Bocco, beki Waziri Salum, kinda Joseph Kimwaga na kiungo Franky Domayo walio majeruhi.

Wakati huo huo kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ukurasa pendwa wa DAKIKA 90 umerejea kivingine kabisa na sasa unapatikana katika link www.amsuni.host56.com ambapo kesho utakuwa kwenye majaribio katika urushaji wa matokeo ya moja kwa moja toka uwanja wa Taifa.
 

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.