Saturday, September 20, 2014

KAVUMBAGU AANZA LIGI KWA GOLI 2, AZAM IKISHINDA

Posted By: Unknown - 7:20 PM

Share

& Comment


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEilRTAb-JN5NeUIVFkwgRQkKnxJ4s0AZc4tGpq5XoNhT3BPSlp2chTkUkdFp3qMX2sgL4nF4BoumfbSk5VIei0fAbkPHLd4aL5CxSfFy9CGl6Xr5rUYVpmG9I1h0U584mma92UVoBxRAIYe/s1600/KAVU+SHANGWE.jpg

Mshambuliaji mpya wa Azam FC Didier Kavumbagu leo ameanza vyema msimu wa ligi kuu ya vodacom baada ya kutikisa nyavu mara mbili katika ushindi wa goli 3-1 wa Azam FC walioupata mbele ya Polisi Morogoro mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex.

Katika mchezo ho wa kwanza wa ligi kuu ya vodacom Azam FC walianza kuandika goli kupitia kwa Kavumbagu katika dakika ya 14 akiunga pasi ya Kipre Tcheche.

Baada ya goli hilo kuingia Polisi Morogoro walipoteana na kupelekea Azam FC kutawala vilivyo mchezo wa leo ambapo Kocha Omeg alivyanya mabadiliko matatu katika kikosi chake toka katika kiosi kilichopoteza kwa Yanga katika mchezo wa Ngao ya jamii.

Kocha Omog alimwanzisha kiungo Mudathir Yahya, beki Gardiel Michael sambamba na kipa Aishi Salum Manula wakichukuwa nafasi za Leoanel, Erasto Nyoni na Mwadini Ally.

Azam FC walicheza vyema eneo la kati na kupelekea Polisi Moro muda mwingi kubaki nyuma na mnamo dakaka ya 23 beki Aggrey Morrice aliiandikia Azam FC goli la pili na kuipeleka Azam FC mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Kipindi cha pili kilianza taratibu huku Azam FC wakiendelea kutawala eneo la kati la uwanja na mnamo dakika ya 60 Nahoda Bakari aliianikia goli la kwanza Polisi Morogoro.

Kuingia kwa goli hilo lilipelekea kujiamini kwa Polisi Morogoro ambapo amanusura waandika goli la pili kufuatia mpira wa Salum Machaku kugonga mwamba akiwa amebaki yeye na kipa.

Alikuwa Kavumbagu aliyetimisha kalamu ya magoli kwa kufunga goli safi katika dakika ya 89 na kuipa ushindi wa kwanza Azam FC katika msimu huu wa ligi wa goli 3-1.

Azam FC leo iliundwa na: Aishi Salum, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, David Mwantika, Aggrey Morrice, Mudathir Yahya, Himid Mao/Mcha Khamisi, Kipre Bolue, Didier Kavumbagu, Salum Aboubakari, Kipre Tcheche/Faridi Mussa 

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.