Thursday, September 25, 2014

OMOG: NATAKA UBINGWA WA BARA

Posted By: kj - 9:43 AM

Share

& Comment

 http://m.habarileo.co.tz/images/resized/images/joseph-omog25_300_150.jpg
KOCHA Mkuu wa Azam FC, Joseph Omog amepania kuhakikisha timu yake inatetea ubingwa wake wa Tanzania Bara msimu huu baada ya kuweka mikakati ya kushinda kila mechi watakayocheza.

Akizungumza na gazeti hili jana, Omog alisema endapo timu yake itacheza vizuri na kupata ushindi katika kila mchezo, itakuwa ndiyo njia pekee nyepesi ya kutetea ubingwa wao na kuendelea kutawala ligi ya Tanzania.

“Unajua nimegundua msimu huu timu nyingi zimejiandaa na ushindani umekuwa mkubwa sana, kwa hiyo ni lazima kuhakikisha kila mechi tunashinda ili kujirahisishia kazi ifikapo mwishoni mwa msimu,” alisema Omog.

Raia huyo wa Cameroon alisema ni vigumu kwa sasa kuwaza ub ingwa, lakini ushindi unamsaidia kujua mwelekeo wa timu yake katika mbio hizo za kuwania taji la pili la Tanzania Bara akiwa kocha wa Azam FC.

“Siwezi kuongelea ubingwa kwa sasa kwa sababu ligi ndiyo kwanza inaanza. Hata zile timu ambazo zimefungwa mechi zao za kwanza, zinaweza kuwa mabingwa kama zitabadilika ila sisi kama Azam lengo letu ni kucheza kwa jihad katika kila mechi ili tupate ushindi,” alisema Omog.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya Ruvu Shooting keshokutwa, Omog alisema utakuwa mchezo mgumu kwa sababu wapinzani wao walipoteza mchezo wa ufunguzi wakiwa nyumbani hivyo hawatakubali kuona wanapoteza mchezo huo kirahisi.

“Lakini pamoja na hayo, tumejipanga kuhakikisha tunakabiliana na ushindani huo na kupata ushindi. Tumeingia kambini juzi jioni wachezaji wote wapo katika hali nzuri na hatuna majeruhi akitoa John Bocco na Salim Waziri ambao wanajulikana siku nyingi,” alisema Omog.

Omog aliyejiunga na Azam mwanzoni mwa mwaka huu kuchukua nafasi ya Stewart Hall, amejijengea sifa kubwa baada ya kuiwezesha timu hiyo kubeba taji la kwanza la ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu.



chanzo: HABARI leo

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.