Saturday, October 4, 2014

AZAM FC WAPATA SARE SOKOINE, MCHEZO WA 37 BILA KUPOTEZA

Posted By: kj - 7:31 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam FC hii leo wamepunguzwa kasi baada ya kwenda sare ya bila kufungana katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Azam FC wakicheza kwa mara ya kwanza nnje ya uwanja wake wa Azam Complex katika msimu huui  wa ligi (2014/15) wamefanikiwa kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi katika michezo 37 mfufululizo.

Katika mchezo wa leo kocha Omog alimpuzisha kiungo Mudathir Yahya huku akimuanzisha Gaudency Mwaikimba ambaye leo hakuwa katika kiwango chake kilichozoeleka hususani linaokuja suala la Azam FC kucheza nnje ya Azam Complex.

Sare hiyo ya leo inaendelea kumuweka Azam FC katika usukani wa ligi ambapo msimamo unaweza kubadilika hapo kesho kama Mtibwa sugar atafanikiwa kumfunga Mgambo shooting katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom utakao chezwa katika uwanja wa Manungu complex.

Azam FC leo: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Said Moradi, Agrey Morrise, Kipre Bolue, Himid Mao, Salum Aboubakari, Gaudency Mwaikimba, Didier Kavumbagu na Kipre Tcheche.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.