Unajua huu mchongo ukoje? Hawa jamaa wanazungumza Kifaransa ndio maana wanaelewana sana. Tchetche raia wa Ivory Coast alisema katika mechi tatu walizocheza mpaka sasa mabeki wa timu pinzani wamekuwa wakimkamia kwa kuhakikisha hafungi lakini Kavumbagu amekuwa mjanja kwa kukaa sehemu nzuri ambazo amekuwa akimpatia pasi safi kufunga mabao.
“Unajua kwangu kikubwa ni Azam kushinda kama umefuatilia katika mechi zetu mabeki wamekuwa wakijua kwamba naweza kuwafunga sasa wanahakikisha sifungi lakini wakati wakiniangalia mimi Didier amekuwa akijua kukaa sehemu safi ambayo nikimpa pasi anafunga kirahisi.
“Unajua mawasiliano yetu uwanjani yamekuwa rahisi kutokana na wote kuzungumza lugha moja ya Kifaransa ukiacha hilo kama unavyojua Didier ni mzuri katika kumalizia ukimpa pasi tatu, mbili hawezi kukosa ni mshambuliaji mzuri,”alisema mchezaji huyo ambaye Yanga waliwahi kummezea mate.
chanzo: mwanaspoti
0 Maoni:
Post a Comment