Saturday, October 25, 2014

AZAM FC WAPOTEZA MBELE YA JKT RUVU

Posted By: kj - 7:05 PM

Share

& Comment

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRFvYWlmm-9uasWd_EeCpYJh8Mz9BTP2Xi_54KSnMZRspvbpNHDppnYxmM4cFXFf5Y5swI1bvghfaamQyH3v6ZWZonqmWMO2Mp9DsKMjw6cbELI1KRlnZOUATLqo0qctZziIu3_wd4x2Q/s1600/KAMUNTU.jpg
Wachezaji wa JKT Ruvu wakishangilia goli (Picha toka kwa Bin Zubeiry)
JKT Ruvu imekuwa timu ya kwanza kuifunga Azam FC baada ya michezo 38 ya ligi kuu ya vodacom kucheza bila kupoteza na imekuwa timu ya pili kuifunga Azam FC katika uwanja wake wa Azam Complex uliopo Chamanzi jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya Tanzania BAra ambapo Azam FC iliingia uwanjani bila ya nyota wake Kipre Herman Tcheche ulimalizika kwa JKT Ruvu kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Azam FC hii leo waliuanza mpira taratibu huku wakimiliki mpira kwa kiasi kikubwa ambapo kwa muda mrefu wachezaji wa JKT Ruvu walionekana kuganda katika eneo lao na huku wakitumia mipira ya kushtukiza katika kupeleka mashambulizi.

JKT Ruvu waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 43 kupitia kwa Samuel Kamitu na kuipeleka JKT Ruvu mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa upande wa Azam FC huku Farid Mussa Maliki akienda benchi na nafasi yake kuchukuliwa na Khamis Mcha Viali mabadiliko ambayo hukubadilisha mwelekeo wa mchezo.

Jackson Chove na beki za JKT Ruvu iliyokuwa inaongozwa na Minja ilifanya kazi nzuri ya kuzima mashambulizi ya Azam FC ambao hii leo walionekana kukosa ubunifu katika eneo la ushambuliaji.

Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Azam FC walikuwa nyuma kwa goli 1-0 na kupelekea kushuka kwa nafasi moja na kuwaacha Mtibwa Sugar wakiwa kileleni mwa ligi.

Azam FC leo: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Morice, Said Morad, Erasto Nyoni, Himid Mao/Mwaikimba, Kipre Bolue, Didier Kavumbagu, Salum Aboubakari, Farid Mussa/Mcha.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.