Saturday, October 18, 2014

AZAM WAENDELEZA WIMBI LA USHINDI

Posted By: kj - 7:17 PM

Share

& Comment

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhi9JFNotQuEOoUXD4BYuirSQm7gzNc4p_sDPZzW_us0opUUxDQbHTuhN6MxqAM8kzGgfU4Q96GrXC7ySfZ0NYOYdcnSF0feNDAPs2sGIV8bAh8f8qRLWoBI_M9yOJlgXVWELJHf4yacJ4/s1600/AGGREY+BAO.jpg
Mabingwa wa Tanzania Bara Azam FC leo wameendeleza ubabe wao kkwa Mbeya City katika uwanja wa Sokoine baada ya kuichapa goli 1-0 na kuwa mchezo wa 38 wa ligi kuu ya vodacom wakicheza bila ya kupoteza.

Katika mchezo huo ulioanza saa kumi na nusu goli la Azam FC lilipatikana katika dakika ya 23 kupitia kwa Beki Aggrey Morrice akipiga mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja hadi kwenye nyavu za Mbeya city.

Kabla ya Mchezo wa leo Mbeya city walikuwa hawajapoteza mchezo wowote ule wala kuruhusu nyavu zao kuguswa katika michezo mitatu ya wali ambapo walitoka suluhu na JKT Ruvu kabla ya kuwafunga Coastal union goli 1-0 na kisha kutoka suluhu na Ruvu shooting.
Azam FC inakuwa tinmu pekee mpaka sasa kuotka na ushindi mbele ya Mbeya city katika uwanja wa Sokoine, ambapo hajapoteza mchezo wowote wa mwingine wa ligi toka apande ligi kuu msimu uliopita ukiondoa michezo miwili dhidi ya Azam FC. (mmoja msimu uliopita na mwingine msimu huu).
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgR5hyphenhyphenebDEg_iFn-eJ2gIej91w0VYuXUIWJhD9TuDJUhyphenhyphenMqxlO8sXuPPFOOftWAT0wCjWDhIiEzVX0KWiEPYkMqMAf04JFgZjFCpHOAJE1jYARjy-Q0_BQDc-xR9nXZhh_3oa0kPoq4tyA/s1600/BALOU+NA+MWAGANE.jpg
Katika mchezo wa leo Azam FC waliingia kwa dhamira ya kutafuta matokeo zaidi na kocha Omog alimuanzisha Erasto Nyoni katika nafasi ya kiungo hivyo kuimarisha zaidi eneo la ulinzi.

Ushindi wa leo Azam FC wamefikisha pointi 10 baada ya michezo minne waliyocheza na mchezo unaofuata utachezwa Azam Complex wikiebdi ijayo dhidi ya JKT Ruvu.

Azam FC leo: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Morrice, Said Moradi, Erasto Nyoni, Himid Mao, Kipre Bolue, Didier Kavumbagu/Gaudence Mwaikimba, Salu Aboubakari, Kipre Tcheche/Mudathir Yahya

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.