Wednesday, November 5, 2014

AZAM FC WAINGIA KAMBINI BILA YA TCHECHE, GARDIEL AANZA MAZOEZI

Posted By: Unknown - 7:25 PM

Share

& Comment

Azam Fc imeingia kambini leo jioni katika Hostel za Azam Complex, Chamazi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa siku ya Jumamosi, dhidi ya timu ya Coastal Union kutoka mkoa wa Tanga.

Beki Erasto Nyoni, aliyepata ajali juzi baada ya gari lake kugongana na mwendesha pikipiki, maarufu kama bodaboda anatarajiwa kuanza mazoezi jioni ya leo, baada ya kumaliza kesi yake Polisi.

Azam FC itaendelea kumkosa mshambuliaji Kipre Tchetche aliyekwenda nyumbani kwao, Ivory Coast kwa matatizo ya kifamilia, wakati beki Gardiel Michael ameanza mazoezi baada ya kukosa mechi dhidi ya Ndanda kwa kuwa majeruhi.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.