Friday, November 7, 2014

AZAM FC: LAZIMA TUWAWALAZE COASTAL

Posted By: kj - 5:48 AM

Share

& Comment

KLABU ya Azam FC imeahidi kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani katika kuondoka na pointi tatu katika mchezo wao dhidi ya Coastal Union utakaochezwa kesho.

Katika michezo miwili iliyopita, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara wamefanya vibaya baada ya kukubali kichapo kutoka kwa JKT Ruvu bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wao wa Azam Complex, na kichapo kama hicho kutoka kwa Ndanda FC katika mchezo wa wiki iliyopita mjini Mtwara.

Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa Azam FC, Jaffari Idd alisema matokeo hayo mabaya hayajawakatisha tamaa kwa vile wamejipanga kuhakikisha wanashinda.

“Kikosi kimerejea salama na tayari kimeanza mazoezi tukitarajia kufanya vizuri kwenye uwanja wetu wa nyumbani, tuna imani tutashinda kwa vile wachezaji wana hasira ya kupoteza katika michezo miwili hivyo wataonesha juhudi kushinda,” alisema Idd.

Alisema kinachohitajika na mashabiki wao kutokata tamaa na matokeo yaliyopita kwani ni sehemu ya mchezo.
Alisema bado hawako mbali kwa pointi kiasi cha kuwakatisha tamaa kwani wataendelea kupambana kwa ajili ya kutetea taji la ubingwa wa Ligi Kuu.

Kikosi hicho ambacho hufundishwa na Kocha Mkuu Joseph Omong, kinakabiliwa na baadhi ya majeruhi kama vile mchezaji wao tegemeo John Bocco na Kelvin Friday.

Idd alisema wachezaji hao wameshaanza mazoezi ya kujifua na itategemea kocha atakavyowaona kama wataweza kucheza. Wengine kama David Mwantika na Lionel Saint Preux nao pia wanaendelea vizuri.


CHANZO: HABARI LEO

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.