Monday, November 3, 2014

KALLY AACHI NGAZI, AENDA KUONGEZA UJUZI

Posted By: kj - 9:09 PM

Share

& Comment


Kocha msaidizi wa Azam FC Kally Ongala amejiuzuru kuifundisha Azam FC, baada ya kupata nafasi ya kwenda kujiendeleza na elimu ya ukocha nchini Uingeleza.

Kally kabla ajawa kocha msaidizi wa Azam FC alipata kuwa mchezaji wa Azam FC amefikia uwamuzi huo wakuacha kazi ya ukaimu kocha kwa lengo la kwenda kujiendeleza nchini Uingeleza.

Kwa mujibu wa kauli ya ofisa habari wa Azam FC Japhar Iddi Maganga Kally aliwakilisha barua ya kuomba kuacha kazi kwa viongozi wa Azam FC na uongozi kukubali ombi lake hilo.

Kally ambaye ameitumikia Azam FC kwa takribani miaka mitano akiwa kama mchezaji na kocha msaidizi, anaicha Azam FC wakiwa wametoka koupoteza michezo miwili mfululizo ya ligi kuu ya vodacom.

Kally alikuwa miongoni mwa waliounda benchi la ufundi ambalo liliiongoza Azam FC kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa ligi kuu bila ya kupoteza mchezo wowote ule msimu wa 2013/14 na likuwa kwenye benchi la ufundi lililo iwezesha Azam FC kufika hatua ya fainali ya kombe la Kagame (inayoshirikisha klabu bingwa Afrika mashariki na kati) ikiwa inashiriki kwa mara ya kwanza katika mwaka 2012.

Kwa mujibu wa Maganga bado unogozi wa Azam FC haujateuwa nani atakae chukuwa nafasi ya Kally Ongala, na ungozi bado unashughulikia wa kuchukuwa nafasi yake.

Ila kwa mujibu wa uoni wa mtandao huu kuna kila dalili ya Ibrahim Shikanda akachukuwa nafasi hiyo.

Kally anakuwa kocha wa pili wa Azam FC kuondoka ndani ya miezi mitatu, kwani Azam FC ilishaondokewaga na kocha wa kikosi cha timu ya vijana ambapo nafasi yake imesha jazwa.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.