Baada ya tukio hilo, Nyoni, beki wa Taifa Stars alitoka kwenye gari lake aina ya Toyota Grande Mark 11 GX 110, akaanza kujitahidi kukimbia kutokana na lundo la bodaboda kuanza kumfukuza wakitaka kuchukua sheria mkononi, hali iliyomtia hofu.
Walimfukuza hadi kufika eneo la Kijitonyama ambako alikwama baada ya kuligonga gari hilo la GPL na alipoteremka kwenye gari, wakaanza kumshambulia kama mwizi.
Nyoni alishambuliwa na lundo la madereva Bodaboda, lakini akafanikiwa kukimbia huku wakiendelea kumpiga na hata watu walipojitokeza kumsaidia, waliendelea kumpiga bila huruma.
GARI LA BEKI ERASTO NYONI WA AZAM FC (KULIA) LIKIWA KATIKA ENEO LA KIJITONYAMA BAADA YA KUKWAMA KUTOKANA NA KULIGONGA GARI LA GLOBAL PUBLISHERRS. |
Beki huyo wa Azam FC alionekana kama anakimbilia kituo cha Polisi cha Kijitonyama Mabatini, lakini hakufanya hivyo na madereva hao wa Bodaboda walipomnasa walikuwa wakimshambulia kama mwizi naye alijaribu kujitetea na alipozidiwa, alitokomea kusikojulikana.
CHANZO: SALEH JEMBE BLOG
0 Maoni:
Post a Comment