Na Saada Salim, DAR ES SALAAM
KOCHA Msaidizi wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC, Kalimangonga Sam Daniel Ongala ‘Kali Ongala’ amethibitisha kujiondoka katika benchi la ufundi akidai anarejea nchini Uingereza kwa ajili ya kuendelea la elimu ya Ukocha.
Kali alisajiliwa mwaka 2009 kama mchezaji wa ndani akitokea nchini Sweden na baadaye aliondoka nchini Uingereza kwa ajili ya kusomea ukocha na kurejea akiwa kocha msaidizi wa timu hiyo.
Kocha huyo aliliambia BIN ZUBEIRY, kuwa ameamua baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya Ndanda FC siku ya Jumapili aliongea na uongozi wa timu hiyo kuwaeleza azma yake ya kujiondoa katika benchi la ufundi.
“Nilikutana na viongozi na kuwaeleza azma yangu ya kujiondoa katika benchi la ufundi, kwa kurejea darasani. Januari au Februari mwakani nitaondoka hapa nchini, kuelekea Uingereza ambako nilipata elimu yangu ya awali ya ukocha,” alisema.
Kali aliongeza; “Siondoki Azam kwa ajili ya matokeo mabaya ya mechi mbili, kwani kupoteza mechi ni jambo la kawaida, lakini nahitaji wadau waelewe nimeamua kurudi shuleni, kuongeza elimu ya ukocha,” alisema.
Alisema anatarajia kuchukuwa muda wa mwaka mmoja nchini humo kwa ajili ya kupata elimu hiyo ya ukocha, pia anaweza kurejea kuendelea kukinoa kikosi cha timu hiyo endapo uongozi utahitaji huduma yake.
“Tanzania nyumbani pia, kwa hali hiyo nitarajea kufundisha timu yangu, kama watanihitaji lakini ninachokiangalia zaidi ni maslahi, kwani ninachoenda kufanya ni kupata sura mpya ya ujuzi wa ukocha,” alisema.
Kali ni mtoto wa mwanamuziki nyota wa zamani nchini, Dk Remmy Ongala (marehemu), ambaye alikuwa ana asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), lakini amefuata uraia wa mama yake, Muingereza.
CHANZO: BIN ZUBEIRY
KOCHA Msaidizi wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC, Kalimangonga Sam Daniel Ongala ‘Kali Ongala’ amethibitisha kujiondoka katika benchi la ufundi akidai anarejea nchini Uingereza kwa ajili ya kuendelea la elimu ya Ukocha.
Kali alisajiliwa mwaka 2009 kama mchezaji wa ndani akitokea nchini Sweden na baadaye aliondoka nchini Uingereza kwa ajili ya kusomea ukocha na kurejea akiwa kocha msaidizi wa timu hiyo.
Kocha huyo aliliambia BIN ZUBEIRY, kuwa ameamua baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya Ndanda FC siku ya Jumapili aliongea na uongozi wa timu hiyo kuwaeleza azma yake ya kujiondoa katika benchi la ufundi.
“Nilikutana na viongozi na kuwaeleza azma yangu ya kujiondoa katika benchi la ufundi, kwa kurejea darasani. Januari au Februari mwakani nitaondoka hapa nchini, kuelekea Uingereza ambako nilipata elimu yangu ya awali ya ukocha,” alisema.
Kali Ongala ameondoka Azam FC |
Alisema anatarajia kuchukuwa muda wa mwaka mmoja nchini humo kwa ajili ya kupata elimu hiyo ya ukocha, pia anaweza kurejea kuendelea kukinoa kikosi cha timu hiyo endapo uongozi utahitaji huduma yake.
“Tanzania nyumbani pia, kwa hali hiyo nitarajea kufundisha timu yangu, kama watanihitaji lakini ninachokiangalia zaidi ni maslahi, kwani ninachoenda kufanya ni kupata sura mpya ya ujuzi wa ukocha,” alisema.
Kali ni mtoto wa mwanamuziki nyota wa zamani nchini, Dk Remmy Ongala (marehemu), ambaye alikuwa ana asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), lakini amefuata uraia wa mama yake, Muingereza.
CHANZO: BIN ZUBEIRY
0 Maoni:
Post a Comment