Kally Ongala aliachia ngazi siku ya jumatatu na mtandao huu wakati inaripoti kujiuzulu kwa Kally ilieleza kuwa huenda Shikanda akachukuwa nafasi hiyo na ndivyo ilivyotokea baada ya uongozi wa Azam FC kufikia uwamuzi huo.
Katibu Mkuu wa Azam FC, Idrissa Nassoro, alilitabainisha kuwa, tayari wameshapata mrithi wa nafasi hiyo iliyoachwa na Kally.
“Kuanzia sasa Ibrahim Shikanda ndiye atakayekuwa kocha wetu msaidizi mpaka hapo Kali atakapomaliza masomo yake japokuwa hatujui atamaliza lini,” alisema Nassor.
Michuano hiyo ya Kagame ilifanyika nchini Rwanda mwaka huu, na Azam FC waliteuliwa kushiriki michuano hiyo baada ya Yanga kujitoa ikiwa imesalia siku chache kuanza kwa michuano hiyo.
Ibrahim Shikanda amekuwa mchezaji na sehemu ya benchi la ufundi la Azam Fc kwa takribani miaka 5 sasa toka ajiunge na Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara akitokea Kenya.
0 Maoni:
Post a Comment