
Meneja wa Azam FC Jemedari Said amesema Wawa amefuzu vipimo vya Afya alivyo fanyiwa leo na kesho anatarajia kusiani mkataba wa kuitumikia Azam FC.
“Wawa tumeshamfanyia vipimo leo na kesho tunatarajia kusaini naye mkataba, tunamsubiri wakala wake atawasili kesho alfajiri kisha tutasaini mkataba,” alisema Saidi.
Wawa alikuwa akiichezea El Merreikh ya Jamhuri ya Sudan ambapo amemaliza mkataba wake. Anatua Azam kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine wa kigeni Ismailla Diarra wa Mali, aliyeoneshwa mlango wa kutokea.
Wawa anakuwa mchezaji wa tatu wa Ivory Coast kusajiliwa Azam akitanguliwa na pacha, mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo Kipre Cheche na kiungo Kipre Balou. Azam imefanya mabadiliko kujiimarisha baada ya kutetereka na kupoteza mechi mbili kwenye ligi.






0 Maoni:
Post a Comment