Saturday, November 8, 2014

WANAO MUHITAJI KIPRE ANDAENI MPUNGA WA KUTOSHA

Posted By: kj - 5:44 AM

Share

& Comment

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/70607000/jpg/_70607976_ivorians_.jpg
Siku chache kabla ya dirisha dogo dirisha dogo la usajili, Azam FC imefunguka kuwa ipo tayari kuwauza wachezaji wake Shomari Kapombe, Kipre Tchetche na Mwadini Ali endapo kutatokea klabu nyingine inayoweza kutoa dau zuri.

Hatua hiyo inakuja hivi karibuni, baada ya kuripotiwa kuwa Kipre anaweza kuondoka klabuni hapo kuelekea nchini Malaysia, Sri Lanka au katika Klabu ya Sofapaka ya nchini Kenya.

Katibu Mkuu wa Azam FC amesema, Idrissa Nassor, alisema kuwa kama kuna timu itawahitaji wachezaji wao watawauza lakini kwa dau la uhakika kutokana na viwango vyao.
Nassor alisema kuwa mpaka sasa hakuna mchezaji wa kikosi hicho ambaye amemaliza mkataba wake ili kuweza kuondoka katika klabu hiyo labda mpaka pale msimu utakapokuwa unamalizika.

“Kama kuna timu yoyote ya ndani au nje itawahitaji wachezaji wetu kama Kipre Tchetche, Shomari Kapombe au Mwadini Ali hatuna tatizo, kikubwa ni maelewano, ingawa wachezaji hawa wana mkataba,” alisema Nassor.

CHANZO: SALEH JEMBE

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.