Wednesday, December 31, 2014

AZAM FC KUFUNGUA NA KCCA MAPINDUZI CUP

Posted By: kj - 9:18 AM

Share

& Comment

http://azamfc.co.tz/sites/default/files/imagecache/slides/BOCCO.JPG
Mabingwa waq ligi kuu ya Tanzania Azam FC wanataraji kuelekea Zanzibar kwa ajili ya michuano ya kombe la Mapinduzi ambapo watafunguwa kwa kucheza dhidi ya KCCA siku ya ijumaa (januari mbili mwakani).

Kwa mujibu wa ratiba inaonyesha michuano hiyo itaanza hapo kesho kwa michezo mitatu huku mchezo wa Azam FC ukichezwa kesho kutwa saa mbili usiku ikiwa ni baada ya mchezo dhidi ya KMKM na Mtende.

Azam FC wamepangwa katika kundi B sambamba na KMKM, Mtende Rangers na KCCA wakati kundi A lina SC Villa, Yanga, Shaba na Polisi huku kundi C likiwa na Simba SC, Mtibwa Sugar, JKU na Mafunzo.

Mchezo wa pili wa Azam FC utakuwa dhidi ya KMKM takaochezwa januari 4 saa kumi na moja, huku mchezo wa mwisho katika hatua ya makundi ukichezwa januari 6 saa tisa alasiri dhidi ya Mtende.

Kwa mjibu wa Afisa habari wa Azam Fc Japhari Iddi, Azam FC itaenda Zanzibar na kikosi chake chote, na wanatarji kuondoka leo.

Kwa ratiba ya michuano hii tembelea SIB RATIBA

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.