Friday, January 2, 2015

AZAM KUWAKABILI KCCA SAA 11 JIONI

Posted By: Unknown - 9:33 AM

Share

& Comment

Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Azam fc leo saa kumi na moja jioni katika uwanja wa Amani watatupa karata yao ya kwanza katika michuano ya kombe la mapinduzi pale watakapo wakabili mabingwa wa kombe hilo KCCA toka Uganda.

Mchezo wa mwisho kukutana KCCA na Azam fc ilikuwa december 21 mwaka jana jijini Kampala ambapo Azam fc walikubali kichapo cha goli 2-0 toka kwa timu hiyo inayomilikiwa na almashahuri ya Kampala katika mchezo huo wa kirafiki.

Mwanzoni mwa mwaka jana Azam fc walikutana na KCCA katika hatua ya nusu fainali ya kombe la mapinduzi na Azam fc kuchapwa goli 3-2.

Azam fc wameenda Zanzibar na kikosi kamili kwa ajili ya michuano hiyo ambayo Azam fc wanaitumia kama sehemu ya maandalizi na klabu bingwa Afrika na ligi kuu.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.