Azam fc ambao leo walikuja kivingine kulinganisha na michezo iliyopita waliandika goli lao pekee katika dakika ya 34 kupitia kwa Didier Kavumbagu baada ya kazi nzuri ya Majegwa.
Azam FC hii leo walicheza kwa uwelewano mkubwa kulinganisha na mchezo uliopita na kufanikiwa kutengeneza nafasi kadhaa ambapo kama John Raphael Bocco na Kavumbagu wangezitumia vyema basi wangeibuka na ushindi wa zaidid ya goli 3.
Katika mchezo huo Azam FC walimtumia kwa mara ya kwanza Franky Dumayo ambayo ameyaanza vyema makazi yake mapya ndani ya Azam FC.
Domayo na Mudathir Yahya walicheza kwa ulewano mkubwa katika eneo la kati ya uwanja, huku John Bocco na Kavumbagu wakicheza pia kwa uelewano.
Kwa matokeo hayo Azam FC watacheza keshokutwa saa kumi na moja jioni dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa robo fainali.
0 Maoni:
Post a Comment