Saturday, January 24, 2015

AZAM KUENDELEZA YA MSIMU ULIOPITA?

Posted By: Unknown - 10:06 PM

Share

& Comment

Kesho katika uwanja wa Taifa azam fc watakuwa na mchezo dhidi ya simba sc ambapo msimu uliopita azam fc waliibuka na ushindi katika michezo yao yote dhidi ya simba sc.

Oktoba 28 mwaka juzi Azam fc waliwafunga simba sc goli 2-1, goli zote za Azam FC zikifungwa na Kipre Herman Tcheche ambaye mpaka sasa ana magoli 2 msimu huu.

Machi 30 mwaka jana katika uwanja wa taifa Azam fc waliibuka na ushindi wa goli 2-1 magoli ya azam fc yakifungwa na Hamisi Mcha ambaye msimu huu ajapewa nafasi ya kutosha na John Bocco aliyekwisha funga goli 1 msimu huu katika mchezo mmoja aliyo cheza.

Simba sc chini ya Goran Kopunovic haijapoteza mchezo wowote katika michezo 6 aliyoiongoza simba, michezo 5 ikiwa ni ya kombe la mapinduzi huku mchezo mmoja ni wa ligi kuu ya vodacom.

Urejeo wa Aggrey Morise aliyekosa mchezo dhidi ya Kagera sugar unaimarisha safu ya ulinzi ya azam fc, sambamba na urejeo wa Bocco aliyosa mchezo dhidi ya Kagera sugar na dhidi ya stand united unaongeza utamu katika safu ya ushambuliji ya Azam fc.

1 Maoni:

  1. Okwi hakugongana bali kapigwa kipepsi.Tuwe wawazi tu wakuu.

    ReplyDelete

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.