Tuesday, January 6, 2015

TCHECHE AUGULIA MOYONI KUKOSA MAPINDUZI

Posted By: Unknown - 1:23 PM

Share

& Comment

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzOnQIW3VOe1sos3IEEv-YMQ9alpzLZFiTmXWZmbpxEB2ey_UuSs6Bzi25T0ymRNmT6MAFfQuLiGscnzdJoJVY-v17qMGhNufI0s2SdWrV5YbmR3rIZAxSso7PChyz9HaAJagSO0_VkUA/s400/DSC_6007.JPG
STRAIKA wa Azam FC, Kipre Tchetche, ameanza mazoezi madogo juzi Jumapili huku akiwa majeruhi wa enka, lakini anachosikitika ni kuendelea kukosa mechi za Kombe la Mapinduzi zinazoendelea visiwani Zanzibar.

Tchetche raia wa Ivory Coast na mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, yupo Zanzibar lakini ameshindwa kushiriki michuano hiyo kwa kuwa ni majeruhi. Amekosa mechi za hatua ya makundi dhidi ya KCCA waliyotoka sare ya mabao 2-2 na dhidi ya KMKM waliposhinda bao 1-0.

Akizungumza na Mwanaspoti, Tchetche alisema: “Nimeshaanza mazoezi lakini hali yangu bado siyo nzuri nina maumivu ya enka, jambo ambalo linanikosesha raha lakini ndiyo hivyo sina jinsi.

“Nasikitika kukosa michuano hii, hata hivyo naamini Mungu ndiye anapanga, nitarudi kwa kasi.”Hata hivyo Kipre amewapongeza wachezaji wenzake wanaondelea na michuano hiyo.

CHANZO: MWANASPOTI

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.