Katika mchezo huo uliokuwa wa kuvutia hususani katika eneo la katikati ya uwanja kulipo kuwa kumejaa kila aina ya ufundi, Azam fc walipata goli lao katika dakika ya 18 ya mchezo kufuatia nahodha wa KMKM Khamis Ali 'Chichi' kujifunga katika harakati ya kuokoampira wa adhabu uliopigwa na Shomari Kapombe.
Pamoja na Azam fc kupata ushindi huo wa goli moja, wakati mwingi walikuwa wanatafuta mpira ma kama KMKM wangekuwa makini katika nafasi walizo tengeneza basi wangekuwa na uwezo wa kushinda hata goli 3.
Kwa matokeo hayo kundi B linaongozwa oa KCCA walio wafunga Mtende goli 3-0 katika mchezo wa mapema hapo jana na kufikisha pointi 4 sawa na Azam fc wanaoshika nafasi ya 2 huku nafasi ya 3 na ya 4 ikishikiliwa na KMKM na Mtende.
0 Maoni:
Post a Comment