Thursday, February 12, 2015

2000 KUSHUHUDIA AZAM Vs EL0MERREKH, TIKETI KUUZWA KESHO

Posted By: kj - 4:58 PM

Share

& Comment

http://3.bp.blogspot.com/-yrfKUAJV0C0/VNtyPOV_pXI/AAAAAAABdgw/Z-5xBf0Qpos/s1600/azam%2Bshangwe.jpg
Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam FC jana wameweka bayana viingilio vya mchzo kati yao na El0merekh utakao chezwa siku ya jumapili saa kumi na moja jioni katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi.

Kiingilio cha chini ni Tsh 2,000/=, huku kiingilio cha juu ni Tsh 10,000/=, wakati kiingilio kingine ni Tsh 5000/=.

Tiketi za mchezo huo zinatarajiwa kuanza kuuzwa hapo kesho januari 13 mwaka huu na kutakuwa na tiketi 7000 tu.

Uongozi wa Azam FC inawaomba mashabiki wakate mapema tiketi zao, ili kuepuka usmbufu hapo baadae na mchezo huo utaonyeshwa moja kwa moja na Azam TV katika channel yake ya Azam two.

Mchezo huo kati ya Azam FC na El-merekh ya Sudan ni mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ya klabu bingwa Afrika, ambapo Azam FC inashiriki mara ya kwanza.

Azam na El-merekh walikutana mwaka jana katika klabu bingwa Afrika mashariki na kati, ambapo EL-merekh ambao wamewasili mchana wa leo walishinda kwa mikwaju ya penati

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.