Sunday, February 15, 2015

AZAM FC WAICHAPA EL-MEREKH MBILI, BOCCO AINGIA NA GOLI

Posted By: kj - 7:49 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam FC wamefanikiwa kuichapa El-merekh goli 2-0 katika mchezo wa klabu bingwa ya Afrika uliochezwa katika uwanja wa AZam complex jijini Dar es salaan.

Katika mchezo huo ambao Pascal Wawa alikuwa anatekeleza wajibu wake kama inavyotakiwa kwa kufika kwa wakati na kupoka mpira bila kufanya madhambi.

Mchezo huo ulioanza kwa kasi na El-merekh wakicheza kwa kuonana na kusababisha Azam FC kuanza wakiwa nyuma.

Shambulizi la kushtukiza ambapo Salum Aboubakari alimtangulizia Kipre Tcheche na akiwa amebaki na kipa alishindwa kuiipatia goli la kuongoza Azam FC.

Katika dakika ya 9 Didier Kavumbagu aliiandikia Azam fc goli la kwanza akitumima vyema uzembe wa kipa na beki wa El-merekh kwa kushindwa kuoka krosi ya Brian Majegwa.

Kuingia kwa goli hilo kuliwatuliza Azam FC na kuanza kucheza soka la kuonana na huku El-merekh wakipoteza umakni wanapovuka nusu ya uwanja.

Kipindi cha pili El-merekh waliuwanza mchezo kwa kasi na uimara wa Wawa, Aggrey Morice sambamba na Aishi Salum uliwanyima fursa El0merekh kuziona nyavu za Azam fc.

Kocha wa Azam Fc Omog alimpumzisha Franky Domayo katika dakika ya 68 na nafasi yake ikachukuliwa na Himid Mao, kitendo kilicho imarisha eneo la ulinzi la azam fc na kuanza kupiga mipira mirefu kwa Kipre Theche na Kavumbagu.

Dakika ya 76 John Bocco aliingia kuchukuwa nafasi ya Kipre Tcheche na kama alivyofanya dhidi ya yanga, Bocco aliiandikia Azam FC goli la pili katika dakika ya 78 akiunga kichwa cha Didier Kavumbagu ambaye naye aliunga mpira wa kurusha wa Erasto Nyoni na kuipa Azam FC ushindi wa goli 2-0.

Kama Salum Aboubakari angekuwa makini kila anapo ingia katika eneo la hatari la El-merekh basi Azam FC wangeibuka na ushindi wa goli 4-0.

Azam na El-merekh wanataraji kurejeana tena nchini Sudan baada ya wiki mbili.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.