Tuesday, February 3, 2015

AZAM FC WAMALIZA WALIVYOANZA

Posted By: Unknown - 9:45 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam fc wamehitimisha ziara yao nchini DR Congo kwa kichapo cha goli 1-0 toka kwa Don Bosco, wakati katika mchezo wake wa kwanza alikubali kichapo cha goli 1-0 toka kwa wenyeji wao TP Mazembe.

Azam fc inayojiandaa kuwakabili El-merekh ya Sudan katika klabu bingwa Afrika, ilialikwa na TP Mazembe kwa ajili ya michuano mifupi iliyo anza januari 28 na kufikia tamati hii leo.

Azam fc baada ya kukamilisha michezo yake leo, wanataraji kurejea nchini kesho, teyari kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya vodacom dhidi ya Polisi Moro katika uwanja wa Jamhuri, kabla ya jumatano kuwakabili Mtibwa sugar katika uwanja wa Azam.


MATOKEO YA MICHEZO ILIYOCHEZWA KATIKA MICHUANO HIYO

Januari 28, 2015
TP MAZEMBE 1-0 AZAM FC
ZESCO UNITED 1-0 DON BOSCO

Januari 31, 2015
AZAM FC 2-2 ZESCO UNITED
DON BOSCO 1-3 TP MAZEMBE

Februari 03, 2015
AZAM FC 0-1 DON BOSCO
TP MAZEMBE 1-0 ZESCO UNITED

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.