Friday, March 13, 2015

AZAM FC WAISHANGAA TFF NA BODI YA LIGI

Posted By: kj - 2:32 PM

Share

& Comment


Uongozi wa mabingwa wa soka nchini Azam FC umeshindwa kuielewa TFF pamoja na bodi ya ligi kwa kitendo cha kusogeza mchezo wao dhidi ya Ndanda FC hadi siku ya jumatatu ya machi 16 mwaka huu, hali ya kuwa uwanja wa Azam Complex hautakuwa na shughuli yoyote wikiend hii.

Malalamiko hayo yamewekwa katika ukurasa wa Azam FC katika Facebook, huku mtandao wa Bin Zubeiry ukimnukuwa mtendaji mkuu wa Azam FC akilalamika juu ya kitendo hicho.

"Mechi kati ya Azam FC na Ndanda imepangwa kucheza Jumatatu 16/3/2015. Hakuna sababu yoyote ya msingi iliyofanya mechi hii isichezwe kesho Jumamosi na kupelekwa mbele hadi jumatatu.
Uwanja upo Chamazi, timu zipo tayari lakini mechi inapangwa Jumatatu", ili eleza taarifa ya Azam FC katika ukurasa wa facebook.

Katika blog ya Bin Zubeiry inaeleza kuwa Azam FC waliomba mchezo wao uchezwe jumamosi badala ya jumapili, lakini TFF wakaamua kuupeleka mchezo huo jumatatu.

.TFF na bodi ya ligi wamekuwa wakibadili ratiba mara kwa mara na kuwaacha njia panda wadau wa mchezo huo, kwa kushindwa kuielewa ratiba, na kuzibebesha mzigo vilabu.

Azam FC wameshakuwa wajanga wa hili pale TFF walipotangaza kufuta mchezo wa katikati ya wiki siku mbili kabla ya mchezo wakati Azam FC ilikuwa teyari imeshafanya booking ya hotel watakoyo fikia Tanga kwa ajili ya mchezo huo ulioghairishwa siku ya jumatano.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © 2025 CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.