Monday, March 16, 2015

AZAM WAREJEA KILELENI, WAILAZA NDANDA FC

Posted By: kj - 6:41 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam FC wamefanikiwa kurejea kileleni hii leo baada ya kuifunga Ndanda FC goli 1-0, katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Azam complex hii leo.


Katika mchezo huo wa leo Azam FC waliuwanza mchezo taratibu, huku wakitumia muda kuwasoma wapinzani wao waliouanza mchezo kwa kasi na kucheza vyema katika eneo la kati ya uwanja.

Azam FC walitumia dakika 15 kurejesha mchezo katika utawala wao, na kupelekea kutengeneza nafasi kadhaa, ambazo Kavumbagu na Franky Dumayo wakishindwa kuzitumia nafasi hizo.

Katika dakika ya 24, Kipre herman Tcheche alimtoka beki wa Ndanda FC na kupiga pasi ya 'V' iliyomkuta Didier Kavumbagu ambaye aliiandikia goli pekee Azam Fc akimaliza vyema kazi ya Tcheche.

oli hilo lilipelekea Azam Fc kuendelea kutawala mchezo na kutengeneza nafasi ambazo walishindwa kuzitumia na kupeleka mchezo mapumziko azam fc wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili Azam FC walitumia muda mwingi kuzuia huku wakipeleka mashambulizi ya kushtukiza ambayo yalishindwa kuzitumia, huku Ndanda kwa mara kadhaa walifanikiwa kumjaribu kipa wa Azam FC Aish Manula ambaye hii leo alikuwa imara.

Kipindi cha pili Ndanda FC waliutawala mchezo na kupelekea mchezo kumalizika kwa Azam FC kuvuna pointi 3 na kufikisha pointi 33 wakiwa mbele kwa pointi mbili toka kwa yanga sc.

Azam FC leo: Aish Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Aggrey Morice, Mudathir yahya, imid Mao, Franky Domayo/John Bocco, Didier Kavumbagu, Kipre Tcheche/Amri Kiemba na Brian Majegwa

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © 2025 CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.