Sunday, March 15, 2015

WACHEZAJI 10 WA AZAM WAITWA STARS, DOMAYO AKIREJESHWA

Posted By: kj - 3:55 PM

Share

& Comment

 Wachezaji 10 wa azam fc wameitwa katika kikosi cha timu ya taifa kitakachoingia kambini march 22 kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi utakaochezwa marchi 29 mwaka huu.
Wachezaji hao 10 ni kati ya wachezaji 27 waliotangazwa na kocha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) Mart Nooj, ambapo kikosi chake kitakabiliana na Malawi katika uwanja wa CCM Kirumba.

Wachezaji wa Azam FC waliotiwa ni Aishi Manula, Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morice, Franky Domayo, Salum Aboubakari, Amri Kiemba, Khamis Mcha na John Bocco.

Wachezaji wengine walioitwa ni:  Deogratius Munish (Yanga), Mwinyi Haji (KMKM), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Oscar Joshua (Yanga), Abdi Banda na Hassan Isihaka (Simba SC).

Viungo ni Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United), washambuliaji Mwinyi Kazimoto (Al Markhiry - Qatar), Saimon Msuva , Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta (Tp Mazembe - Congo DR) na Juma Luizio (Zesco United - Zambia)

Timu ya Taifa ya Malawi inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza machi 27, 2015 ikiwa na kikosi kamili, wakiwemo wachezaji nane wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini, Msumbuji, Congo DR na Zimbambwe.

Malawi inashika nafasi ya 91 katika viwango vipya vya FIFA Duniani vilivyotolewa mwezi huu, huku Tanzania ikipanda kwa nafasi saba na kushika nafasi ya 100.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © 2025 CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.