Friday, March 6, 2015

JESHI LA NSIMBE VITANI KESHO DHIDI YA JKT RUVU

Posted By: kj - 4:10 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Azam FC kesho watashuka katika uwanja wa Azam complex kuwakabili JKT Ruvu katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu msimu huu.

Azam FC watashuka katika mchezo huo utakao anzaa saa moja usiku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza katika uwanja huo, pale walipo wakaribisha JKT ruvu.

Azam FC inayonolewa na kocha toka Uganda George Best Nsimbe baada ya mwanzoni mwa wiki hii kumtimua kocha Joseph Omog, na huo utakuwa mtihani wa kwanza kwa kocha huyo aliyekuwa msaidizi wa Omog.

Wachezaji wa Azam FC walingia kambini hapo jana kujianda na mchezo huo utakao rushwa moja kwa moja na Azam TV, huku blog hii, sambamba na blog ya Sport in Bongo kupitia kipengele cha SIB DAKIKA 90 kitakuleta matokeo yamchezo huo kila yanapo badilika.

Azam FC watashuka uwanjani kwa dhamira ya kutafuta ushindi ili kupunguza tofauti ya pointi baina yake na vinara wa ligi kuu ya vodacom, Yanga wanao tofautiana kwa point nne.

Kikosi cha Azam FC kikovizuri na kinaendelea na maandalizi yake ya mwisho mwisho ya kusaka pointi tatu muhimu mbele ya wanajeshi hao wa kujenga Taifa.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.