Monday, March 23, 2015

MCHEZO WA MGAMBO NA AZAM WASOGEZWA TENA

Posted By: Unknown - 8:43 PM

Share

& Comment

Wachezaji 12 wa Azam FC waliotiwa katika timu zao za Taifa wamepelekea mchezo kati ya Azam FC na Mgambo shooting kusogezwa mbele ili kupisha michezo ya kimataifa ya kirafiki inayotambuliwa na FIFA mwishoni mwajuma hili.
Wachezaji wote 12 leo wametawanyika kwenda kujiunga na timu zao za Taifa, huku wachezaji 10 walioitwa katika kikosi cha Taifa Stars wakiwa wamewasili leo katika kambi ya timu hiyo inayojiandaa na mchezo dhidi ya Malawi utakao chezwa siku ya jumapili marchi 29 katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza..

Nnje ya hao kumi waengine wawii wameitwa katika mataifa yao, ambao ni Didier Kavumbagu akiitwa katika kikosi cha Burundi na Brianv Majegwa akijumuishwa katika kikosi cha Uganda.

Kutokana na hali hiyo kumepelekea mchezo kati ya Azam FC na Mgambo shooting uliokuwa uchezwe siku ya jumatano marchi 25 kusogezwa mbele.

Wakati huo huo kikosi cha Azam FC kimewasili salama jijini Dar es slaam wakitokea Mkoani Tanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa hapo jana.

Kwa niaba ya uongozi afisa habari wa Azam FC Japhari Iddi Maganga amewashukuru mashabiki wa Azam fcwaliojitokeza katia uwanja wa Mkwakwani na kuwataka waendeleee kujitokeza katika michezo mingine.

Hii ni mara ya pili mchezo huo wa mzunguko wa kwanza kati ya Azam FC na Mgambo shooting kushindwa kufanyika na kusogezwa mbele.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.