Tuesday, March 24, 2015

BOCCO: MBIO ZA UBINGWA BADO UNAENDELEA

Posted By: Unknown - 5:27 PM

Share

& Comment


NAHODHA wa Azam FC, John Bocco amesema ushindi walioupata katika mchezo wao dhidi ya Coastal Union unawapa nafasi ya kuendelea kupambana kutetea taji la ubingwa wa ligi.

Mabingwa watetezi, Azam FC waliondoka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga na hivyo kusogea kwa pointi 36 wakiwa nyuma ya vinara wa ligi, Yanga wenye pointi 37.

Akizungumza jana, Bocco alisema nia yao ni kutetea ubingwa, hivyo wataendelea kujituma kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu kwa kila mchezo uliobaki.

“Nia yetu ni kutetea taji la ubingwa, ndio maana tunapopata ushindi tunafarijika na kuwa na moyo wa kuendelea kupambana kuhakikisha ushindi unabaki kwetu,” alisema mshambuliaji.

Bocco ndiye aliyeifungia timu hiyo bao la ushindi katika mchezo huo wa Tanga. Alisema licha ya mchezo huo kuwa mgumu kutokana na mazingira ya uwanja, walichojali wao ilikuwa ni kushinda na walipambana na kufanikiwa.

Naye Meneja wa timu hiyo, Jemedari Said alisema kikosi hicho kilicheza vizuri na kufanikiwa kuondoka na ushindi.

Said alisema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha wanashinda katika michezo mingine iliyobaki kwa ajili ya kutetea ubingwa kwa msimu mwingine.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi, raundi ya 21 kutakuwa na mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.