Friday, March 27, 2015

SURE BOY KUENDELEA KUKOSEKANA, AKUTWA NA LUNGU LA TFF

Posted By: Unknown - 9:34 PM

Share

& Comment

Kiungo mchezeshaji wa Azam FC Salum Aboubakari "Sure Boy" ataendelea kukosekana uwanjani baada ya kufungiwa michezo mitatu ya ligi kuu ya vodacom.


Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyotolewa leo, Sure boy amekumbwa na rungu hilo kutokana na kitendo cha kurushiana ngumi na mchezaji wa JKT Ruvu, ambpo alizawadiwa kadi nyekundu.

"Nao wachezaji Salum Abubakar wa Azam FC na Richard Maranya wa JKT Ruvu wamepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kila mmoja na kusimamishwa mechi tatu kwa mujibu wa Kanuni ya 37(3) kwa kupigana uwanjani kwenye mechi namba 123 ambapo walitolewa nje kwa kadi nyekundu," ilielelza taarifa hiyo ya TFF.



Sure boy teyari amesha kosa michezo miwili dhidi ya Ndanda FC na Coastal union kutokana na kadi nyekundu aliyoonyeshwa katika mchezo huo kati ya JKT Ruvu na Azam FC.

Vile vile TFF imewapiga faini Ndanda FC kwa kitendo cha mashabiki wake kuwamwagia maji mashabii wa Azam FC katika mchezo uliochezwa Azam complex.

"Mechi namba 132 iliyozikutanisha Azam na Ndanda SC kwenye uwanja wa Chamazi, klabu ya Ndanda imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) baada ya washabiki wake kuwamwagia maji na kuwarushia chupa za maji washabiki wa Azam."

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.