Tuesday, March 10, 2015

TETESI: KITAMBI KUMSAIDIA NSIMBE

Posted By: kj - 3:18 PM

Share

& Comment

ALIYEKUWA kocha wa Ndanda FC, Denis Kitambi ameula kwa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Azam, baada ya kupewa jukumu la kuiongoza timu hiyo.

Habari za uhakika kutoka Azam jana zilisema Kitambi ataanza kazi rasmi leo kwa kushirikaina na kocha Mganda George Nsimbe.

Kitambi alikuwa mwajiriwa wa Azam kama mchambuzi wa masuala ya soka. Azam iliachana na makocha wake Joseph Omog na Ibrahim Shikanda kwa madai ya kushindwa kufanya kazi yao ipasavyo.

Akizungumza na gazeti hili mmoja wa viongozi wa juu wa Azam, alisema uongozi umeamua kumpa Kitambi kazi hiyo.

“Bado tupo kwenye kutafuta kocha, lakini kwa sasa Kitambi atakuwa na timu akisaidians na Nsimbe,” alisema kiongozi huyo.

Omog ndiye aliyeiongoza Azam kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Mei mwaka jana, lakini hakuweza kuipa mafanikio kwenye michuano ya kimataifa.

Mwaka jana ikishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho iliishia raundi ya awali baada ya kufungwa na Ferroviario de Nampula.

Hilo lilijirudia mwaka huu ambapo ilitolewa mapema na El Merreikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda mabao 2-0 nyumbani kabla ya kufungwa mabao 3-0 Sudan.

chanzo: habarileo

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.