Saturday, April 25, 2015

AZAM FC WAENDELEA MBIO ZA KUSAKA NAFASI YA KUWAKILISHA NCHI, YAICHAPA STAND GOLI 4

Posted By: kj - 6:22 PM

Share

& Comment


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara Azam FC, hii leo wamefanikiwa kupta ushindi wa kwanza mkubwa baada ya kuwa na ushindi mwembamba toka wacheze na El-merekh ya Sudan mwezi wa pili mwaka huu.

Azam FC hii leo wamewafunga goli 4-0, Stand united katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Azam complex.

Katika mchezo wa leo ambao azam fc walitawala eneo la kati ya uwanja walianza kupata goli la kwanza katika dakika ya 14 kupitia kwa Brian Majegwa, kufuatia shuti la nnje ya eneo la hatari lililo mshinda mlinda lango wa Stand united.

Azam FC waliandika goli la pili katika dakika ya 37 kupitia kwa Gaudence Mwaikimba akiunga kwa kichwa krosi ya Salum Aboubakari na  kupelekea Azam FC kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Kipindi cha pili Stand united waliongeza umakini katika eneo la kati ya uwanja na kupelekea kocha Geoger Best Nsimbi kumpimzisha Mudathiri Yahya na nafasi yake kuchukuliwa na Bryson Raphaeli.

Mabadiliko hayo yalizaa goli katika dakika ya 63 baada ya wachezaji wa stand kugongana wakati wanajaribu kuzuia krosi na mpira kumkuta Mwaikimba ambapo aliiandikia Azam FC goli la tatu.

Nsimbi alimpumzisha Mwaikimba na Kavumbagu ambapo nafasi zao zilichukuliwa na Kipre Tcheche na Faridi Mussa Maliki, ambapo katika dakika ya 89 walihusika katika upatikanaji wa goli la 4.

Kipre Tcheche katika dakika ya 89 alimuhadaa kipa wa Stand united na kutoa pasi iliyomkuta Faridi Mussa na kuiandikia Azam FC goli hilo la nne.

Kwa matokeo hayo Azam FC inaendelea kumfukuzia yanga katika mbio za ubingwa na kama yanga ataambulia sare ama kupoteza katika mchezo wake wa jumatatu dhidi ya Polisi Morogoro, utafunguwa mwanya kwa azam fc kuendelea kumfukuizia yanga, lakini endapo akishinda yanga basi ndio watakuwa wametwaa ubingwa.a

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.